SAMIA : TUNATAKA UWEKEZAJI UFIKE DOLA BILIONI 15 IFIKAPO MWAKA 2025 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 11, 2023

SAMIA : TUNATAKA UWEKEZAJI UFIKE DOLA BILIONI 15 IFIKAPO MWAKA 2025


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na India katika muendelezo wa Ziara yake ya Kitaifa, New Delhi 10 Oktoba, 2023.


Viongozi, Wafanyabiashara pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na India uliofanyika New Delhi tarehe 10 Oktoba, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na India uliofanyika New Delhi tarehe 10 Oktoba, 2023.





Viongozi, Wafanyabiashara pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na India uliofanyika New Delhi tarehe 10 Oktoba, 2023.

NA SELEMANI MSUYA, NEW DELHI INDIA 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema mikakati ya Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha ifikapo 2025 uwekezaji kutoka kutoka nje kwa mwaka uwe umefikia dola za Marekani bilioni 15, kutoka dola bilioni 5 kwa sasa na kwamba India ni moja ya eneo wanalolitolea macho.

Aidha Rais Samia amewaambia wafafanyabiashara na wawekezaji kutoka India wasipoteze fursa ya kuwekeza Tanzania kwa kuwa ni nchi yenye fursa na amani ya kutosha.

Rais Samia ameyasema Oktoba 10,2013 jijini New Delhi India wakati akizungumza na wafanyabishara na wawekezaji wa nchini India na Tanzania wakati wa Jukwaa la Uwekezaji kati ya India na Tanzania, lilofanyika katika Hotel ya ICT Mourya.

Amesema serikali yake imeweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hivyo anawaomba wake Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali kwani hawatajutia kufanya maamuzi hayo.

Rais Samia amesema uwekezaji wa India nchini Tanzania unaendelea vizuri na kwamba matarajio yao ni kuona unakuwa mara tatu ifikapo 2025, hali ambayo itachangia lengo la kufikia dola za Marekani bilioni 15 kufukiwa mwaka huo kwa ujumla wake 

Amesema Serikali inawakaribisha wawekezaji waje  kuwekeza katika sekta mbalimbali na kwamba serikali imejipanga kuwapa ushirikiano wa kutosha, huku akiwashauri kutumia mifumo ya teknolojia kusajili biashara zao kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).                                                                           

Rais Samia amesema tangu mwaka 1997 Tanzania imepokea uwekezaji kutoka India unaofikia dola za Marekani bilioni 3.87 uliohusisha miradi 675 na kuwezesha upatikanaji wa ajira 61,000 na kuifanya nchi hiyo kuwa kati ya nchi tano kubwa zilizowekeza nchini.

Amesema mikakati ya serikali yake ni kuona India inawekeza mtaji wa wa dola za Marekani bilioni 3 kwa mwaka kutoka dola milioni 300 ya sasa.

"Tunawakaribisha mje kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu sahihi, lengo la kuwa na uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 15 mwaka ifikapo 2025 litafikiwa ikiwemo mchango wa India, niwahakikishie hamtajutia uamuzi wenu kwani kuna fursa nyingi nzuri,"amesema.

Aidha Rais Samia ametoa wito kwa wananchi wa India kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania kama Zanzibar, Kilimanjaro, Ngorongoro, Serengeti na kwingineko, ili kujionea mambo mazuri ya nchi hiyo.

Amesema vivutio hivyo ni baadhi ya faida ambazo mwekezaji atanufaika nazo nchini Tanzania na kwamba hiyo ni moja ya sababu ya kuwaambia hawatajutia kuwekeza nchini.


No comments:

Post a Comment