NA MAGENDELA HAMISI
CHAMA cha ACT Wazalendo kimebainisha kuwa kutokana na kila mwaka Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuibua ubadhilifu wa fedha za Serikali trillion 3.14 na wahusika wakiachwa bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria mwarobaini wake ni kupatikana kwa Katiba Mpya.
Hayo yamewekwa wazi na Waziri Kivuli, Ofisi ya Rais Mipango, Fedha na Hifadhi ya Jamii, Kiza Mayeye wakati akijibu swali baada ya kuichambua Ripoti ya CAG ya mwaka 2022/2023 mbele ya waandishi wa habari na wahariri jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2024.
“Upatikanaji wa Katiba Mpya utasaidia kusimamia sheria vizuri kwa sababu kila ripoti ya CAG inaposomwa haingii akilini kuona madudu yaleyale na wahusika wanaona Tanzania ni kama shamba la bibi wanafanya ubadhilifu wa fedha na hata wakitajwa hakuna wa kuwachukulia hatua,” amesema.
Pia ipitishwe sheria yeyote akitajwa na ripoti ya CAG kufanya ubadhilifu wa fedha za Serikali afungwe mfano China, mtu akipatikana na hatia ya kufanya ubadhilifu anachukuliwa hatua kali zaidi hapa Tanzania ni tofauti hata ripoti ikionesha mtu kafanya ubadhilifu anaachwa sasa hilo ni tatizo,” amesema.
Amesema ripoti hiyo iliyosilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan Machi 28 na kusomwa bungeni Aprili 15, 2024 na ikitarajiwa kujadiliwa katika kikao cha Bunge cha Septemba mwaka huu kuna hoja 10 zinazotakiwa kufanyiwa kazi na Serikali.
Mayeye amesema hoja ya kwanza ni ukuaji wa deni la taifa ambalo limefikia trillion 82.25 sawa na ongezeko la asilimia 15 na kiasi cha trillion 10.94 kimeongezeka kulinganisha na mwaka wa fedha uliopita na athari yake ni kwamba kila kitachokusanywa katika mapato ya Serikali kitakwenda kulipa deni badala ya kutatua shida za Watanzania.
Pia amesema kuongeza kwa deni la taifa kutasababisha ongezeko la mikopo ya biashara yenye masharti mafupi na magumu, ongezeko la kodi kwa watanzania.
ACT Wazalendo wamesema hoja nyingine ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi ni kulipa deni kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii la shilingi tilion 1.4, ili iraisishe kulipwa kwa wastaafu, pia amesema kwa mujibu wa ripoti ya CAG bado Serikali inautitiri wa mikopo ya sh. Tilioni 1.6 ambazo fedha hizo hazijapokelewa na italipwa tangu kusainiwa na si pale ilitolewa hivyo mikataba kama hiyo inatakiwa kupitiwa upya.
No comments:
Post a Comment