HABARI: SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUUNGA MKONO WATOTO WENYE USONJI
Dar es Salaam, 2 Aprili 2025 –
TANZANIA inakadiriwa kuwa na watoto takribani 20,000 ambao wanazaliwa wakiwa na tatizo la usonji kila mwaka ingawa hakuna takwimu rasmi ya idadi ya walio na changamoto hiyo hiyo sasa.
Hayo yamebainishwa leo, na Naibu Waziri wa Afya, Godfrey Molell, wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Usonji Duniani ambayo uadhimishwa Aprili 2, kila mwaka.
Ameongeza kuwa kati ya hao watoto 1416 wanapewa huduma maalum na hiyo inaonesha kuongezeka kwa mahitaji ya msaada wa kipekee kwa kundi hilo.
Hatuwezi kuzuia wazazi kuzaa watoto wenye changamoto hiyo, kikubwa kinachotakiwa ni kubadilisha mtindo WA maisha ikiwemo kuepuka vileo, kula mlo bora
nchini wanakadiriwa kufikia 20,000 huku aSerikali imewataka wazazi na walezi kuacha kuwaficha watoto wenye usonji na badala yake kuwapeleka katika vituo vya huduma ili waweze kupata matibabu na elimu inayostahili.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Usonji Duniani leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Moleli, amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za afya na elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum ili kuhakikisha wanapata fursa sawa kama watoto wengine.
“Tunaendelea kuimarisha huduma kwa watoto wenye usonji kwa kuongeza wataalamu wa afya kama watoa tiba kwa vitendo, physiotherapists na wataalamu wa lugha na matamshi. Pia, serikali inawekeza kwenye shule maalum kwa ajili ya watoto hawa,” alisema Dkt. Moleli.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Dkt. Omari Ubuguyu, alieleza kwa kina kuhusu usonji, akisema kuwa ni hali inayoathiri mfumo wa fahamu na ukuaji wa mtoto, husababisha changamoto katika mawasiliano na mahusiano ya kijamii, na mara nyingi hujitokeza kabla ya mtoto kufikisha umri wa miaka mitatu.
“Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mtoto mmoja kati ya 100 anaathirika na usonji, huku tafiti zikionesha kuwa watoto wa kiume wanaathirika mara nne zaidi ya watoto wa kike. Hapa Tanzania, tunakadiria kuwa kuna watoto wapatao 20,000 wenye usonji,” alieleza Dkt. Ubuguyu.
Ameongeza kuwa, ingawa chanzo halisi cha usonji hakijulikani, wataalamu wanahisi kuwa ni matokeo ya vinasaba na mazingira. “Ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha lishe bora, kufanya uchunguzi wa kiafya kabla na wakati wa ujauzito, na kuepuka vinywaji vyenye kileo kama pombe ili kupunguza hatari ya matatizo ya kiafya kwa watoto wao,” alisema.
Katika maadhimisho haya, serikali imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuboresha huduma kwa watoto wenye usonji, ili kuhakikisha wanapata elimu na matibabu sahihi kwa maendeleo yao na ustawi wa jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment