NA MWANDISHI WETU
STEVE Mengele 'Steve Nyerere' ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao na Mwimbaji wa Injili, Christina Shushu ni kama vile hawashikiki kwa kukusudia kuandika historia kwa kuandaa tamasha kubwa la muziki wa Injili na kuliita Mtoko wa Pasaka.
Mtoko wa Pasaka ni tamasha la Injili litakalifanyika Aprili 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam, wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Pasaka ambapo Steve na Shusho wamejinasibu kuwepo kwa shoo kabambe kutoka kwa wasanii wa muziki huo wa ndani na nje ya nchi.
Pia litakuwa ni sehemu ya kuwaonesha wageni siri ya amani na utulivu inavyojengwa Tanzania kupitia muziki Injili ambao unawaweka pamoja watanzania bila kujali itikadi ya dini.
Kwa mujibu wa Steve Nyerere', tamasha hilo pia litatumika kumuombea dua, Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Tanzania hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Steve amebainisha hayo leo April 8,2025 jijini Dar es salaam wakati akipiga stori na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
Amesema "Maombi yana nguvu kuliko mtutu wa bunduki,maombi yana nguvu kuliko matusi, maombi yana nguvu kuliko kitu kingine chochote ,hivyo siku hiyo tutaliombea Taifa na Rais wetu Mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan"amesema
Sisi tumeona ndani ya mwezi huu(April)kulikua na mambo mengi ikiwemo ramadhani, kwaresma,na sasa tunelekea kwenye sikukuu ya Pasaka,hivyo kuelekea kilele cha sikukuu ya pasaka tutatoa pakeji ya vifaa vya kumsaidia mama mjamzito kujifungua katika Hospitali zote za Wilaya Mkoani Dar es salaam"
Steve Nyerere amempongeza muimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Christina Shusho kwa kuandaa tamasha la mtoko wa pasaka litakalofanyika siku ya pasaka April,20,2025 jijini Dar es Salaam.
"Watakuwepo waimbaji wote nguli wa nyimbo za injili kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania Kenya,Uganda na kwingineko,ambapo watashiriki katika tamasha hilo ambalo halitakua na kiingilio lenye kauli mbiu isemayo "Kwa maombi tutashinda"
Kwa upande wake Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Christina Shushoo,amesema kwamba tamasha la "Mtoko wa Pasaka" ni kuwaleta Watanzania pamoja na raia wa mataifa mengine ili kufurahi kwa pamoja kupitia nyimbo na muziki wa injili.
"Tumealika na watu wa nje ili waje waone siri ya amani ya nchi ya Tanzania, kwani wengi wanajua Tanzania ni nchi ya amani lakini siri ya amani uliyopo hawaijui". amesema
"Waimbaji wengi watakutana na kufurahi lakini kwasababu ni Mwaka wa uchaguzi tutamuombea Mama yetu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazozifanya za kuliongoza Taifa la Tanzania".amesema.
Amesema kuwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao imekua ikifanya mambo mengi ya kijamii,hivyo yeye kama mwanachama wa Taasisi hiyo ameamua kuandaa tamasha la nyimbo za injili siku ya sikukuu ya pasaka April 20,2025 ili kufurahi pamoja na jamii.
No comments:
Post a Comment