PROF LIPUMBA AMUOMBA RAIS SAMIA WAKAE MEZANI KUJADILI UCHAGUZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, April 12, 2025

PROF LIPUMBA AMUOMBA RAIS SAMIA WAKAE MEZANI KUJADILI UCHAGUZI

 


NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi )CUF), Prof Ibrahim Lipumba, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kukaa na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kujadili   changamoto zilizopo kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.


Prof. Lipumba amebainisha hayo, leo Aprili 12, 2025 jijini Dar es Salaam katika mkutano na wananchi uliofanyika kwenye viwanja vya bakhresa, Manzese.


"Wito wangu kwa Rais Samia, aangalie namna ya kukutana na viongozi wa yama vya siasa ili tujadili kwa pamoja matatizo yaliyopo kabla ya kuingia katika Uchaguzi, naamini Mama yetu ni msikivu na katika hili anaweza kulifanyia kazi ipasavyo," amesema.

Alifafanua kuwa wakati Rais Samia anaingia madarakani waliamini kuwa changamoto zikizojitokeza kwenye chaguzi zilizopita zingefanyiwa kazi haraka akidai kwamba Rais Samia aliwahi kusema kuwa hakuna mwenye hati miliki hivyo iko haja ya kufanya mabadiliko.


Prof aliongeza licha kwamba kauli hiyo bado haijafanyiwa kazi, wito wake kwa  Rais afanye mchakato wa kukutana  na viongozi wa vyama vya siasa wajadiliane Kwa pamoja na kupata njia sahihi ya  kuingia katika uchaguzi kila mgombea akiaminj mazingira mazuri yamewekwa ya kushinda.


Amefafanua kuwa mchakato wa kudai Katiba Mpya na Tume Huru ulianza kipindi kirefu hali iliyosababisha, Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Kisanga, Tume ya Jaji Warioba zote zilihitaji kuwepo na misingi ya kidemokrasia na kupendekeza ifanyiwe marekebisho ingawa hadi sasa hakuna mabadiliko ya msingi yaliyofanyika.


Ameongeza kuwa viongozi wa vyama vya siasa mwaka 2014 jijini Dodom walikaa na Rais wa wakati Jakaya Kikwete kujadili mchakato huo na walikubaliana yafanyike mabadiliko madogo na hadi sasa bado mengi hayajafanyiwa kazi.


Prof alisema licha ya madai yao kutofanyiwa kazi vya kutosha hadi sasa ikiwemo kupata Tume Huru ya Uchaguzi kwa maana hata marekebisho yaliyofanyika, wamo baadhi ya wajumbe hawastahili kuwemo lakini hawatasusia uchaguzi.


"Hatuwezi kususia uchaguzi kwa maana naamini njia sahihi ni kushiriki uchaguzi huku tukiendelea kudai madai yetu yafanyiwe kazi, pia CUF bado tunamtambua Rais Samia kuwa ni halali," amesema


Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Othuman Dunga, amesema kuwa hawawezi kupata maridhiano kama hawatakuwa wamoja.


Amesema kwa sasa wanachoka ni utekelezaji wa mabadiliko ikiwemo kupatikana kwa Tume Huru ya Uchaguzi na si kususia uchaguzi.


"Tunapenda kuwaeleza watanzania kuwa Uchaguzi Mkuu ni fursa ya kuleta mabadiliko na mabadiliko yanayokea kwenye sanduku la kura na kususia ni kujikosesha fursa ya kuleta mabadiliko," amesema.


Pia katika mkutano huo, ametangaza rasmi wanachama na wadau wengine wachangie chama kwa ajili ya mchakato wa kufanikisha kufanya vizuri katika Uchaguzi Mkuu.

 Aidha ameongeza kuwa baada ya mkutano huo wataendelea kufanya mikutano nchi nzima na watasimamisha wagombe katika nafasi zote.


No comments:

Post a Comment