RAIS wa Awamu ya Nne ambaye ni Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Jakaya Kikwete amewasilisha ujumbe maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville), Collenet Makoso Anatole.
Anatole alipokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo , Denis Sassou Nguesso ambaye alikuwa kijijini kwao kushiriki mazishi ya kaka yake.
Tukio hilo lilifanyika jijini Brazzaville Aprili 14, 2025 na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.
Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.
![]() |
No comments:
Post a Comment