WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA FALME YA ESWATINI - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Tuesday, April 15, 2025

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA FALME YA ESWATINI


NA MWANDISHI WETU, USWATINI

WAZIRI wa Afya na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Jenista Mhagama leo Aprili 15, 2025 amewasilisha ujumbe maalum kwa Ufalme wa Eswatini ambao umepokelewa na Waziri Mkuu wa Falme hiyo, Russell Mmiso Dlamini jijini Mbabane, Eswatini.


Waziri Mhagama ameushukuru Ufalme wa Eswatini kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri wa Kidiplomasia uliopo baina ya Mataifa hayo mawili.


Waziri Mhagama ameambatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha Tanzania pia katika  Falme ya Eswatini, Ali Ubwa Mussa pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace, Magembe.




No comments:

Post a Comment