CHALAMILA AWAPA MAAGIZO DAWASA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 9, 2025

CHALAMILA AWAPA MAAGIZO DAWASA


NA MWANDISHI WETU


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira (DAWASA) mkoani humo kuanza mchakato wa kuzalisha umeme utakaotumika katika mashine za kusambazia maji ili kupunguza gharama.


Chalamila amebainisha hayo mapema leo wakati akikagua mradi wa maji  ambao umegharimu Shilingi billioni 36.8  na kwa Kibamba ukiwa umetumia Bil. 4.

Ameongeza kuwa kwa sasa Dawasa inatumia bil. 2 kuilipa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) bil ya umeme, hivyo inaweza kuepuka gharama hiyo ikiwa itazalisha  umeme wake na Tanesco itumike kusambaza tu.


"Kuona mradi huu umeanza kufanya kazi , kwetu ni mafanikio makubwa na tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa mradi huu.


"Hivyo huu si muda wa kudanyanyana kama sehemu kuna tatizo, kiongozi husika anatakiwa kusema ili Serikali itoe fedha, nikigundua kuna kiongozi hajasema ukweli kama kuna sehemu kuna tatizo ili wananchi wasaidiwe na nikabaini nitaanza na yeye," amesema.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,, Lazaro Twange, amesema kwamba kukamilika kwa mradi wa maji Kibamba  kumefanikisha kuondoa changamoto ya ukosefu ya maji katika Kata za jimbo hilo.


Pia Diwani wa Kata ya Kwembe, Nicolus Batiligaya amesema mwaka 2020,  kata yake ilikuwa na ukosefu wa maji na sasa wananchi wake wanapata huduma hiyo kwa asilimia 90.

"Natoa shukrani kwa Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ujenzi wa  miundombinu ya maji ambayo imeboresha maisha ya wananchi wangu kupata maji safi na salama na kuwepo utofauti mkubwa na miaka mitano iliyopita, " amesema.

No comments:

Post a Comment