RC DAR AMTAADHARISHA FUNDI MWENYEJI UJENZI WODI YA WAZAZI, UPASUAJI ZAHANATI YA MPIJIMAGOHE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 9, 2025

RC DAR AMTAADHARISHA FUNDI MWENYEJI UJENZI WODI YA WAZAZI, UPASUAJI ZAHANATI YA MPIJIMAGOHE


NA MWANDISHI WETU


MKUU wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemtaadharisha fundi ujenzi, Yassin Juma kufanya marekebisho haraka la sivyo atapelekwa kujenga milango ya Magereza.


Fundi huyo mwenyeji ambaye amepewa tenda ya ujenzi majengo wodi ya Upasuaji na Mama na Mtoto katika Zahanati ya MpijiMagohe, Mbezi Manispaa ya Ubungo Dar es Salaam, baadhi ya maeneo yameonekana kuwa na kasoro.


Chalamila amefunguka hayo, leo Mbezi jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Ubungo Jimbo la Kibamba.


"Ukiondoa taaluma yangu, pia ninauelewa wa masuala ya ufundi, hivyo kwa kuangalia tu, yapo baadhi ya makosa ambayo tayari nimeelekeza uyafanyie kazi, nitarudi tena kimyakimya nikikuta hujarekebisha itabidi upelekwe gerezani  maana kule kuna milango imeharibika," amesema.


Naye Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Aron Kagaurumjuli, amesema kwamba ujenzi wa  majengo hayo ambayo yanagharimu Shilingi milioni 615 utakamilika mwezi huu.


"Hii ni moja ya Hospitali 18 ambazo zimejengwa katika Manispaa ya Ubungo ikiwa Kata ya Mbezi na inatarajia kuhudumia wakazi 108, 446 na baadhi ya wakazi wa Kibaha mkoani Pwani, amesema


*Kwa sasa mradi huu wa  pili ulioanza Nov 28, 2024 umefikia asilimia 65 na utakamilika mwezi huu wa nne," amesema.

Katika ukaguzi huo, Chalamika aliweka jiwe la msingi katika Zahanati hiyo.


No comments:

Post a Comment