Na Asmah Mokiwa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Gofu cha Wanawake (TLGU), Anita Siwale amesema maandalizi ya timu ya taifa ya wanawake ya mchezo huo kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yamekamilika.
Mashindano hayo yanayoshirikisha nchi za Afrika Mashariki na Kati yanatarajiwa kufanyika, Lusaka, Zambia Juni 3 hadi 5 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Siwale alisema timu hiyo imefanya maandalizi ya kutosha na wanatarajia kurudi na ushindi katika mashindano hayo.
Alisema,"Timu imejiandaa vizuri na tunauhakika wa kurudi na ushindi, kwani wachezaji wako vizuri, wamefanya mazoezi ya kutosha".
Wachezaji wanaounda timu hiyo ni pamoja na Madina Idd ambaye ni nahodha wa timu, Hawa Wanyeche, Ayne Magombe na Angel Eaton.
Nchi zinazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi, Ethiopia, Tanzania na Zambia ambazo ni wenyeji wa mashindano hayo.
mwisho.
No comments:
Post a Comment