Na Jane Edward, Arusha
Wataalamu
wa kitengo Cha kudhibiti na kuzuia ufisadi na rushwa kutoka taasisi za
umma na binafsi nchini wamepatiwa mafunzo yakusaidia taasisi zao katika
kubaini ubadhirifu unaofanywa kwa kutumia mbinu za kiuchunguzi.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyija jijini Arusha wa mapambano dhidi ya ufisadi,Rushwa na ubadhilifu .
Rais
wa chama cha wataalamu wa udhibiti,ufisadi,Rushwa na Ubadhirifu (ACFE)
Stella Cosmas anasema wamekutana kujadili namna bora ya kuzuia na
kupambana na ubadhirifu na masuala ya Rushwa nchini katika taasisi za
ndani.
Amesema
lengo ni kuisaidia serikali katika kupambana na makosa ya kiufisadi na
Rushwa ambapo wameweza kufanya upelelezi mkubwa katika kuhakikisha
Tanzania inaondokana na vitendo vya Rushwa.
"Sisi
ni wapelelezi wa ndani na ni wataalamu kabisa ambao tuna vyeti ambapo
cheti ni Cha Kimataifa na kinapatikana katika nchi 125 na makao makuu ya
chama yapo Marekani"Alisema Stella
Aidha
amesema katika siku za Mkutano watatoa elimu kwa wataalamu kutosubiri
matukio yatokee ndiyo wapeleleze badala yake wapate utaalamu wa kugundua
viashiria kabla havijatokea.
Amesema
wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kupiga vita masuala ya rushwa na
wao wanahakikisha wanaiunga mkono kwa kuendelea kupinga vita vitendo
hivyo ambavyo vinaikwamisha Serikali ya Rais Samia Suluhu katika
maendeleo.
Nao
baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Gladness Msuya afisa viatarishi na
ubora kutoka mamlaka ya bandari nchini anasema vyanzo vya rushwa
vinabadilika kila mara na hivyo mafunzo kama haya yatasaidia kuendana na
teknolojia ili kutumia mbinu mpya na kuweza kuzuia viashiria vya rushwa
na ubadhirifu kwa wakati.
"Sisi
ndiyo Wataalamu tunaotegemewa kuondoa viashiria hivi vya rushwa na kama
tutakuwa na mafunzo mbadala kila mara ni wazi Taasisi hizi zitafika
mbali kimaendeleo kwani rushwa, ubadhirifu ni Adui wa ustawi wa
maendeleo"Alisema Gladness
Bruno
mchopa ni mshiriki kutoka kitengo Cha uchunguzi katika taasisi ya
kifedha CRDB Bank anasema zipo teknolojia mbalimbali wanazotumika katika
kugundua viashiri mapema na kuzifanyia kazi.
Rais
wa chama cha wataalamu wa udhibiti ufisadi Rushwa na ubadhilifu Stella
Cosmas akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Bruno Mchopa Kutoka kitengo Cha uchunguzi CRDB Bank akizungumza na waandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment