Mkurugenzi
wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania, Kelvin Nyema, akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya lugha za alama kwa wanafunzi na
wakufunzi wa chuo cha afya Sumbawanga mkoani Rukwa chini ya ufadhili wa
taasisi ya Nos Vies en Partage (NVep) inayofadhiliwa na Rais na Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation,Mark Bristow.
Mmoja wa wakufunzi wa alama za mikono akitoa mada wakati wa mafunzo hayo
Mkuu
wa Chuo cha afya na Sayansi Shirikishi, Dk. Emmanuel Mwilonga akisoma
taarifa fupi ya maendeleo ya chuo hicho kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa
ni Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa , Christina Mzena
Katibu
Tawala wa mkoa wa Rukwa, Christina Mzena akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo ya lugha za alama kwa wanafunzi na wakufunzi wa chuo cha
afya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Washiriki wa mafunzo hayo katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Bi.Christina Mzena
Taasisi
ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) imeendesha mafunzo ya siku
tatu ya wanafunzi na wakufunzi wa chuo cha Maafisa tabibu kilichopo
mjini Sumbawanga mkoani kuhusu matumizi ya alama za vidole kwa viziwi.
Mafunzo
haya yamefanyika kutokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya
Nos Vies en Partage (NVep) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji
Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation,Mark Bristow, akiwa nchini
hivi karibuni alikabidhi msaada wa dola 10,000 kwa taasisi ya TAMAVITA
kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye
ulemavu.
Akifungua mafunzo hayo, Katibu wa Shirikisho la vyama
vya watu wenye Ulemavu mkoani Rukwa (Shivyawata), Elina John, alisema
kuwa mwitikio wa watu wenye ulemavu kujitokeza na kupata huduma za afya
katika hospitali, vituo vya afya na zahanati umetajwa duni kutokana na
wataalamu wengi wa afya kutokuwa na elimu ya alama za vidole hivyo
kushindwa kuwahudumia kikamilifu na kutibu maradhi yanayowasumbua.
Alisema
kutokana na uelewa duni wa mawasiliano kwa njia ya alama za vidole kati
ya wataalamu wa afya na viziwi wanaokwenda kupata huduma kwenye
hospitali na vituo vingine vinavyotoa huduma ya afya umesababisha viziwi
kukosa matibabu au kutibiwa maradhi wasiougua.
"Hapa kwenye
hospitali ya rufaa ya mkoa kuna mwenzetu mmoja alipewa madawa ya ugonjwa
asiougua......sasa haya mafunzo yatasaidia sana kujenga uelewa kwa
wataalamu hawa lakini pia viziwi watapewa tiba sahihi", alisisitiza
Elina John.
Awali, Mtendaji mkuu wa TAMAVITA, Kelvin Nyema
alisema kukosekana kwa ujuzi wa mawasiliano miongoni mwa wagonjwa
(Viziwi) na wataalamu wa afya hivyo kukosa huduma stahiki pindi
wanapofika hospitalini hivyo ndio maana waliona kuna umuhimu wa kutoa
mafunzo wanafunzi wa mwaka wa tatu ili baada ya kuhitimu waweze kusaidia
kutatua changamoto hiyo.
Naye, Katibu Tawala wa wilaya ya
Sumbawanga, Christina Mzena aliyefungua mafunzo hayo aliwasihi wataalamu
hao wa afya kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi yao na kupunguza
malalamiko yasiyo na tija kutoka kwa wagonjwa.
Thursday, November 10, 2022
New
BARRICK YAFANIKISHA MAFUNZO YA MATUMIZI YA ALAMA ZA VIDOLE KWA VIZIWI RUKWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment