Na Mwandishi wetu, Iringa
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameipongeza
Makumbusho ya Taifa, kwa kutoa elimu ya utalii kidigital.
Mhe.
Waziri alizitoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Utalii
yajukanayo kama Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kihesa
Mkoani Iringa.
Vile vile ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa
kuendelea kuhifadhi historia adhimu ya vita vya MajiMaji ambapo kuna
Makumbusho maalum ya kumbukizi ya vita hivyo mjini Songea.
"Naipongeza
sana Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi historia
adhimu ya nchi yetu na kuitangaza kidigital" amesema Mhe. Waziri.
Maonesho hayo yamewaleta pamoja wadau mbalimbali wa masuala ya utalii kwa ajili ya kutoa elimu na kuhamasisha utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumvusho ya MajiMaji Bi Rose Kingwe akitumia kishikwambi kutoa elimu ya utalii.
No comments:
Post a Comment