WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa,
kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa usambazaji maji kwa wananchi
na kuagiza zoezi hilo pamoja na uchimbaji wa visima katika maeneo
mbalimbali liwe endelevu.
Mheshimiwa
Majaliwa amekagua visima katika eneo la Tabata Relini na Mwananyamala
Komakoma jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Novemba 10, 2022), ambapo
ameshuhudia usafishwaji wa kisima pamoja na zoezi la usambazaji maji.
Visima
hivyo ni miongozi mwa visima 197 vilivyochimbwa na Serikali mkoani Dar
es Salaam ambapo kwa sasa 160 vimefufuliwa na kutoa lita milioni 29.4
kwa siku, Maji hayo yameunganishwa katika mfumo na hivyo kupunguza
changamoto ya maji.
Waziri
Mkuu ameuagiza uongozi wa Bonde la Wami Ruvu pamoja na Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) waendelee kufanya
tafiti kubaini maeneo yenye maji mengi na kuchimba visima na kuyaingiza
katika mfumo.
Mheshimiwa
Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulinda maeneo yote yenye
vyanzo vya maji pamoja na kuyatumia vizuri maji yanayopatikana ili
kukabiliana na tatizo la upungufu wa maji hususani katika kipindi hiki
cha ukame.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma
ya maji safi na salama katika mikoa yote nchini likiwemo jiji la Dar
es Salaam.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inatekeleza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani
ili kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma hiyo karibu na
maeneo yao ya makazi. Amewataka waendelee kuiamini Serikali yao kwa
sababu imedhamiria kuwatumikia.
Awali,
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika kukabiliana na changamoto ya
upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali nchini wizara imejipanga
kuchimba mabwawa kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua na kuyaingiza
katika mfumo.
Waziri
huyo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
kwa kuwawezesha kupata mitambo ya kuchimba visima na hivyo kukabiliana
na upungufu wa maji. “Tutashinda site kuhakikisha maji yanapatikana kwa
wananchi.”
Mahitaji
ya maji katika mkoa wa Dar Es Salaam ni lita milioni 544 kwa siku na
uzalishaji maji kwa siku ni lita milioni 520 katika kipindi ambacho
kiwango cha maji katika Mto Ruvu kinakuwa katika hali ya kawaida, hivyo
kuwa na upungufu wa lita zaidi ya milioni 24.
Hata
hivyo katika kipindi hiki ambacho kiwango cha maji kimepungua katika
Mto Ruvu uzalishaji wa maji nao umepungua na kufikia lita milioni 300
kwa siku, hivyo kusababisha upungufu wa lita milioni 244.
Hivyo
baada ya kuingiza lita milioni 70 kutoka katika mradi wa visima vya
Kigamboni na lita milioni 29.4 kutoka katika mradi wa visima vingine 160
vya jijini Dar es Salaam sasa upungufu wa maji ni lita milioni 145 kwa
siku, hivyo kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya
maeneo jijini humo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akishuhudia
usafishaji wa visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na
kuunganishwa kwenye mfumo wa huduma maji Tabata Kisiwani wakati wa ziara
yake ya kukagua upatikanaji wa maji kwenye visima mbalimbali katika
Jiji la Dar es Salaam ili kuona ni kwanamna ga DAWASA pamoja na Wizara
ya Maji wameweza kushughurikia changamoto ya upatikani wa maji katika
Jiji hilo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipata maelezo
kutoka kwa Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kuhusu namna
walivyofanikisha kusimama pamoja na DAWASA kuchimba visima na kufufua
visima 197 ambapo mpaka sasa visima vipatavyo 160 vinatoa maji mpaka
sasa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu ya kukagua visima katika Jiji la Dar
es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na
viongozi wa Wizara ya Maji, DAWASA pamoja na Wananchi wa Tabata Kisiwani
alipofanya ziara ya kukagua visima vitakavyoweza kupunguza makali ya
upatikanaji wa maji kwenye Jiji la Dar es Salaam
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso wakipata maelezo kutoka kwa Afisa
Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu uzalishaji wa maji
kwenye Kisima cha Tabata Kisiwani ikiwa ni utekelezaji wa kufufua na
kuchimba visima vitakavyoweza kupunguza ukali wa mgao wa maji katika
Jiji la Dar es Salaam
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmasi kuhusu hali
ya upatikanaji wa maji kwenye mto Ruvu, Wami pamoja na kwenye visima
wakati wa ziara ya Waziri Mkuu ya kukagua visima vitakavyoweza kupunguza
ukali wa mgao wa maji katika Jiji la Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam,Jenerali Mstaafu, Davis Mwamunyange.
i
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),
Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) wakati alipokagua visima vya
dharura vinavyosafishwa na kufufuliwa na kuunganishwa kwenye mfumo wa
huduma ya maji kwa wananchi katika eneo la Mwananyamala Kwa Makoma
jijini Dar es salaam , Novemba 10, 2022. Wa nne kulia ni Waziri wa Maji,
Jumaa Aweso, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Jenerali
Mstaafu Davis Mwamunyange na wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Dar es salaam, Kate Kamba.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na
viongozi wa Wizara ya Maji, DAWASA pamoja na Wananchi wa Mwananyamala
kwa Makoma alipofanya ziara ya kukagua visima vitakavyoweza kupunguza
makali ya upatikanaji wa maji kwenye Jiji la Dar es Salaam
Waziri
wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Mwananyamala kwa
Makoma wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokagua
utekelezaji wa kufufua na kuchimba visima vitakavyoweza kupunguza ukali
wa mgao wa maji katika Jiji la Dar es Salaam
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso wakipata maelezo kutoka kwa Afisa
Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu uzalishaji wa maji
kwenye Kisima kilichopo Mwananyamala kwa Makoma ikiwa ni utekelezaji wa
kufufua na kuchimba visima vitakavyoweza kupunguza ukali wa mgao wa
maji katika Jiji la Dar es Salaam
Kisima kilichopo Mwananyamala kwa Makoma
No comments:
Post a Comment