
Kijana
Pinisto Nzali (20) mkulima anayeishi Kidete mkoani Morogoro amefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya
kuchapisha mtandaoni taarifa yenye kuharibu hadhi ya Rais Samia Sulubu
Hassan na Jakaya Kikwete.
Na Karama Kenyunko
KIJANA
Pinisto Nzali (20) mkulima anayeishi Kidete mkoani Morogoro amefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya
kuchapisha mtandaoni taarifa yenye kuharibu hadhi ya Rais Samia Sulubu
Hassan na Jakaya Kikwete.
Mshtakiwa Piniston pia anashtakiwa kwa kosa la kushindwa kusajili laini ya simu iliyokuwa ikimilikiwa na mtu mwingine.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa
serikali Sylivia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luboroga imedaiwa,
Oktoba 8, 2022 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mshtakiwa
alichapisha taarifa yenye kuharibu heshima au hadhi ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Katika
taarifa hiyo inadaiwa, mshtakiwa kupitia mtandao wa Tiktok alichapisha
video inayomuonesha Rais Samia akiimba jambo ambalo halikuwa la kweli.
Mshtakiwa
pia anadaiwa kuchapisha taarifa inayofanana na hiyo ikimuonesha Rais
Mstaafu wa Awamau ya Nne, Jakaya Kikwete akiimba kosa alilolitenda
Oktoba 10, 2022 huku akijua kuwa jambo hali siyo la kweli.
Aidha
katika shtaka la mwisho, inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba
1, 2022 na Oktoba 20, 2022 mshtakiwa alitumia laini ya simu ambayo awali
ilikuwa inamilikiwa na Benjamani Chaji bila kutoa taarifa ya mabadiliko
ya umiliki kwa mtoa huduma.
Mshtakiwa
amekana mashtaka hayo na amerudishwa mahabusu mpaka kesho kesi hiyo
itakapotajwa atajwa kwa ajili ya kueleza hatua upelelezi ulipofikia
No comments:
Post a Comment