Na John Walter-Manyara
Vijana
wenye vipaji kutoka kanda ya Kaskazini Manyara, Arusha,
Kilimanjaro,Tanga pamoja na kanda ya kati Dodoma na Singida, wametakiwa
kuwa wabunifu na nidhamu ili kutimiza malengo yao.
Hayo
yamesemwa Novemba 14,2022 na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati
Super Brand Limited David Mulokozi wakati akizindua Tamasha la kusaka
vipaji linalojulikana kama (Strong Talent Search) yaliyoandaliwa na
Smile FM redio pamoja na Mati super Brand Limited kupitia kinywaji cha
Strong dry Gin.
Akizungumza na vijana mbalimbali kutoka mikoa
hiyo waliochukua fomu za ushiriki, Mulokozi amesema kuna vijana wengi
wenye vipaji lakini wanakosa sapoti na kuishia kurekodi kwa gharama
kubwa kazi zao na kuziweka katika mitandao ya kijamii bila faida,
lakini kupitia tamasha hilo wengi watafika mbali.
Amesema
Platform hii ni fursa kubwa kwa Wasanii kwani watu wengi huwategemea
katika kutuliza stress zao kwa kuburudika huku wao wakiingiza kipato.
Ameongeza
kuwa kwa watakaofanikiwa kupitishwa na majaji watafundwa maadili
mbalimbali ya msanii aweje na Kampuni hiyo itawasiadia kwa kila jambo.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi wa Smile Fm Redio Jamal Mteri, Mchujo wa kwanza
utaanza rasmi Novemba 19, 2022 katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
No comments:
Post a Comment