Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeandaa warsha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
wapato 97 kutoka kwenye vyuo kumi ambavyo ni Chuo kikuu cha Dar es
Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi, IFM, NIT, Mwalimu Nyeere, TIA, Mzumbe,
Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo chaMipamgo MNMA, ISW na Chuo cha Maji
ambapo vyuo hivi vinapatikana kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro
na Dodoma.
Akizungumza
wakati wa kufungu mafuzo hayo ya siku tatu Mkuu wa Idara ya Maarifa,
Utafiti na Uchambuzi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Catherine
Kasimbazi alipowwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi
amesema warsha hii imejikita katika kuongesza ushiriki wa wanafunzi wa
kike katika nafasi za uongozi na ngazi mbalimbali za maamuzi kwa
kuwaelimisha kuhsu masuala ya uongozi ili waweze kufahamu miongozo, sera
na kanuni zinazoongoza Serikali ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Pia
amesema mafunzo haya yatawasaidia wale ambao ni viongozi kuendelea kuwa
bora zaidi na kuweza kuendesha Serikali zao kwa ushirikiano mkubwa na
kuwa chachu ya mabadiliko kiungozi na kuongeza ushiriki wa Wanafunzi
wengi zaidi wa kike kushika nafasi za uongozina ngazi za maamuzi.
Kidunia,
Takwimu za Interparliamentarian Union (IPU) zinaosesha kuna wanawake 21
ambao wakuu wa nchi na wakuu wa Serikali na kwa upande a afrika
tumewahi kuwa na marais watano wanawake ambao ni aliyekuwa Rais wa
Malawi Joyce Banda, aliyekuwa Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf,
aliyekuwa rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim, rais kutoka Ethiopia
Sahle-Work Zewde na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tania Samia Suluhu
Hassan.
Pia
amesema kwa takwimu hizo zinaonesha dadi Januari 2021 kidunia maspika
wa bunge ni asilimia 20.9, Manaibu spika wanawake wanawake ni asilimia
28.3 na wabunge wanawake katika nchi zote walikuwa ni asilimia 25.5
ambapo ni ongezeko la asilimia 42.2 kutoka asilimia 11.3 mwaka 1995.
Amesema
Takwimu za utafiti uliofanywa na TGNP wa kuangalia ushiriki wa wanawake
katika ngazi za maamuzi kwenye mihimilimitatu na vyama vya siasa
unaonesha kuwepo kwa matumaini hasa kutokana na nia ya dhati ya Serikali
ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Sulihi Haasan kutaka
kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi.
Ni
matarajio yangu kuwa warsa hii itajenga viongozi wanawake imara watakao
enda kupunguza pengo la kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi
sio tu vyuoni bali hadi kwenye nafasi nilizotaja bali kwenye nafasi
zenye kufanya maamuzi yatakayosaidia wanawake pamoja na makundi
yaliyopembezoni na jamii kunufaika na rasilimali za taifa.
Amesema
wanacho waliofoka kwenye warsha hiyo wapo kwa niaba ya wanawake na
jamii kubwa waliyoiacha katika maeneo yao hivyo ni muhimu kuyatendea
haki yale yote watakaoyojifunza ili kuyafanyia kazi wa kushirikisha
wananchi ili kuweza kuwainua na kufikia mabadiliko chanya
wanayoyatamani.
Mkuu
wa idara ya Maarifa, Utafiti na Uchambuzi Catherine Kasimbazi akisoma
hotuba wakati wa kufungua warsha kwa wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu
wapato 97 kutoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma. Bi
Catherine alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi
inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022
katika ukumbi wa TGNP Mabibo.
No comments:
Post a Comment