Hili ndo eneo ambalo wavuvi haramu wanaendesha Shughuli uvuvi haramu ambapo kutokana na operesheni imepungua.
Mfuko wa Samaki zilizoharibika zilizotelekezwa wakati operesheni wa Askari wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Ruaha wakati walivyofanya operesheni eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi 'Afande Sele' akionesha Mtumbwi ulioharabiwa na Askari wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Ruaha wakati walivyofanya operesheni eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi akizungumza na waandishi habari kuhusiana Uvuvi haramu unaofanyika kwenye Mto Ruaha na Hifadhi ya Ruaha katika eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

* Wananchi waingiza mitumbwi na nyavu kwenye hifadhi
Na Chalila Kibuda
WAKATI
serikali ikiweka mkazo wa kutoendesha shughuli za Uvuvi katika hifadhi
imekuwa tofauti kwa wananchi wa Bonde la Usangu/Ihefu kuendesha
shughuli hizo ndani ya hifadhi ya Ihefu na Mto Ruaha.
Hali
hiyo imebainika baada Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na
Taarifa (MECIRA) kutembelea Mto Ruaha kwenye Bonde la Usangu/Ihefu eneo
la Matopetope-Ikoga wilaya ya Mbarali mkoani.
Akizungumza
eneo la Matopetope ambapo shughuli za Uvuvi zinafanyika Mragibishi na
mdau wa Mazingira Seleman Msindi 'Afande Sele' amesema kuwa wananchi
kuendesha shughuli za uvuvi ndio chanzo cha kukauka mto Ruaha na kupotea
kwa Uoto wa asili bonde la Usangu/Ihefu.
Msindi
amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yametokana na shughuli za
kibinadamu na kusababisha mto Ruaha kukauka katika kipindi kufupi cha
kiangazi.
Amesema
kuwa uvuvi haramu kwenye mto Ruaha haukubaliki kutokana na maji hayo
yanashughuli za kiuchumi ya kuzalisha umeme kwenye vituo vya Mtela
,Kidantu pamoja na kihansi.
Aidha
amesema kuwa wananchi wanaingiza mitubwi na kufanya uvuvi haramu na
miti ya mtumbwi imekatwa kwenye hifadhi ya Ruaha Bonde la Usangu/Ihefu.
No comments:
Post a Comment