Na Mwandishi wetu, Tanga
WAFANYABIASHARA
wadogo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Horohoro na
Lungalunga ,wametaka serikali za Tanzania na Kenya, kuondoa vikwazo vya
kibiashara ,hasa baada ya kukamilika miundombinu ikiwepo barabara ya
Tanga- Horororo.
Barabara la lami ya Tanga- Horohoro, imejengwa na Serikali ya Marekani kupitia miradi ya malengo ya milenia (MCC).
Wakizungumza
na mwandishi habari hizi, katika mpaka huo, baadhi ya wafanyabiashara
wadogo wa Kenya na Tanzania, walitaka serikali za Kenya na Tanzania,
kuendelea kupunguza vikwazo ili biashara iwe rahisi zaidi baina ya nchi
moja hadi nyingine, hasa ya mazao, mifugo na bidhaa za ndani.
Joseph
Mwanganya mfanyabishara mdogo wa Kenya kaunti ya Lungalunga, amesema
licha ya serikali za Afrika mashariki kuwa na miundombinu bora mipakani
lakini, bado changamoto kuwa ni vikwazo vya kibiashara.
“Sisi
kama wafanyabiashara tunataka uhuru wa kufanya biashara hasa hizi
ndogondogo turuhusiwe kuingia katika nchi hizi mipakani na kupitisha
biashara ndogondogo hasa hizi za mazao,” amesema.
Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Duga Maforoni, Horohoro, Tanzania, Zahoro Juma, amesema
kwa sasa upande wa Tanzania biashara zimeimarika sana kutokana na uwepo
wa barabara nzuri ambayo inarahisisha usafirishwaji wa bidhaa mbali
mbali.
“Kuna vikwazo vidogovidogo vya kiforodha lakini.,kubwa
biashara zinakwenda vizuri hivi sasa kutoka Tanga hadi Horororo unatumia
saa moja tofauti na miaka ya nyuma tulikuwa tunatumia saa sita kwa
kilomita 65 tu,” amesema.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba
amesema serikali inajitahidi kupunguza vikwazo kwa wafanyabiashara
wadogo katika mpaka huo na biashara zimeimarika sana tofauti na miaka ya
nyuma.
“Wafanyabiashara wadogo tunawaruhusu kufanyabiashara kilometa 10 ndani ya Tanzania na Kenya bila vikwazo,“ amesema.
Amesema
hivi Sasa miundombinu imeimarika hasa barabara hivyo ni fursa kwa
wafanyabiashara wadogo kuitumia na Serikali imetenga maeneo ya
uwekezaji,ikiwepo maeneo ya viwanda na masoko ya bidhaa mbalimbali
ikiwepo mifugo.
Saturday, November 12, 2022
New
WAFANYABIASHARA WADOGO TANZANIA NA KENYA WAELEZA MANUFAA YA MRADI WA BARABARA TANGA-HOROHORO WATAKA KUONDOLEWA VIKWAZO MIPAKANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment