WAWEKEZAJI WENGI WA ITALIA WAMEONESHA NIA YA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA-BALOZI LOMBARDI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, November 15, 2022

WAWEKEZAJI WENGI WA ITALIA WAMEONESHA NIA YA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA-BALOZI LOMBARDI

 

Na Said Mwishehe
BALOZI wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi ameeleza
kwamba wawekezaji wa nchi yao wameonesha nia ya kuja
kuwekeza Tanzania baada ya Jukwaa la Biashara na
Uwekezaji baina ya nchi hizo mbili lililofanyika Septemba
27–30, 2022 kuanza kuleta matokeo chanya.

Amesema wawekezaji wengi walioko Italia wako tayari
kuwekeza katika maeneo ya kilimo, miundombinu ,uchumi wa
bluu pamoja na kubadilishana maarifa kwenye nyanja kadhaa
kwa lengo la kukuza uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza leo Novemba 14,2022 kwenye Hoteli ya Hyatt
jijini Dar es Salamaa, Balozi Lombardi wakati alipokuwa
akielezea Wiki ya Vyakula vya Kitaliano sambamba na
utamaduni wa nchi hiyo ameweka wazi baadhi ya wawekezaji
wa nchi yao wameonesha nia ya kuja kuwekeza hapa nchini
na hilo ni jambo la faraja kwa nchi hizo.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaalika wafanyabiasha na
wajasiriamali wa Tanzania kuitembelea nchi ya Italia kwa
lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika nyanja
mbalimbali ikiwemo fursa zinazoptikana katika uchimbaji wa
madini pamoja na sekta ya viwanda.

Balozi Lombardi amesisitiza kumekuwa na ushirikiano wa
muda mrefu kati ya Tanzania na Italia hivyo ni wakati
muafaka sasa wa kujifunza mambo yenye tija katika
kuongeza uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja na
mataifa hayo kwa ujumla.

Kuhusu wiki ya utamaduni wa Italia amesema ni maalumu
kwa ajili ya kuonesha tamaduni mbalimbali za nchi hiyo huku
akifafanua baadhi ya tamaduni zinafanana na za Tanzania
hasa kwenye baadhi ya vyakula.

"Tuna wajumbe wanaokuja kwa ajili ya programu za
kubadilishana uzoefu hasa katika sekta ya chakula,"
amesema na kubainisha kuwa wanafanya hivyo kuadhimisha
"Wiki ya Vyakula vya Kiitaliano Duniani," inayofanyika
kuanzia Novemba 14 hadi Novemba 20, 2022, kote
ulimwenguni.

Kwa upande wake mmoja wa Watanzania ambaye ni
mjasiriamali anayefanya biashara na Waitaliano amesema
wanafurahia wiki hiyo kwani wanajifunza utamaduni wa
Waitaliano kuanzia chakula na vitu wanavyofanya kwenye
nchi yao.
“Kwetu sisi ni fursa na sio kwenye utamaduni wa cahakula tu
bali hata kwenye masuala ya biashara , bahati nzuri
wametualika kwenda Italia Machi mwakani kwa ajili ya
kupeleka utamaduni wetu.Sisi na Waitalia mambo mengi

tunafanana.Kwenye biashara ambayo tunashirikiana na Italia
ni nyanja nyingi ikiwemo sekta ya madini na bidhaa za ngozi.”Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi(katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusu Wiki ya Utamaduni ya Italia inayoanza leo Novemba 14 hadi Novemba 20 mwaka huu ambayo pia huadhimishwa duniani kote.Katika wiki hiyo kwa hapa nchini kutakuwa na matukio mbalimbali yanayoelezea utamaduni wa watu wa nchi hiyo ukiwemo wa vyakula.Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Hyatt Alexander Eversberg na kushoto ni Meya wa Jiji la Fermo Paolo Calcinaro.Meneja Mkuu wa Hyatt jijini Dar es Salaam Alexander Eversberg(wa kwanza kulia) akizungumzawakati akimkaribisha Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi(wa pili kulia) wakati wa kuelezea Wiki ya utamaduni wa nchi ya Italia iliyoanza leo Novemba 14-20,mwaka huu.Wengine katika picha hiyo ni Meya wa Jiji la Fermo Paolo Calcinaro(wa pili kushoto) pamoja na Albeto Monachesi .
Meya wa Jiji la Fermo lililopo nchini Italia Paolo Calcinaro(wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusu wiki ya utamaduni wa Italia ambayo imeanza leo Novemba 14 hadi Novemba 20 mwaka huu na wiki hiyo inaadhimishwa duniani kote.




Matukio mbalimbali kwenye picha wakati wa utambulisho wa wiki ya Utamaduni wa Italia ambayo imeanza leo Novemba 14 na inatarajia kumalizika Novemba 20 mwaka huu.Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi ameeleza kwa kina kuhusu utamaduni ya nchi hiyo na namna ambavyo wanaendelezea kupitia wiki hiyo.

No comments:

Post a Comment