JESHI LA POLISI LAWAONYA WAZAZI, LAHIMARISHA ULINZI - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Sunday, March 30, 2025

JESHI LA POLISI LAWAONYA WAZAZI, LAHIMARISHA ULINZI


NA MWANDISHI WETU


JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa wito kwa  wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao hawaendi maeneo mbalimbali kusherehekea Sikukuu ya eid wakiwa peke yao bila ya uangalizi.


Imebainishwa kuwa kuwaacha watoto peke yao bila uangalizi wa wazazi kunaweza kusababisha wakapata ajali au kufanyiwa vitendo viovu vitakavyoweza kuathiri maisha yao.


Leo, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Mulilo Jumanne Mulilo, akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema licha ya jeshi hilo kujipanga vema kukabiliana na vitendo viovu, wazazi nao wanapaswa kuwalinda watoto hususani katika kipindi hiki cha kusherehekea Sikukuu ya Eid.


"Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani na asitokee yeyote kujaribu kufanya uhalifu kwani tutamshughulikia ipasavyo," amesema Kamanda SACP Mulilo.


Pia ametanabaisha kuwa fukwe zote ulinzi, umehimarishwa pamoja na pembezoni mwa mji na nidhahiri sikukuu ya Eid itasherehekewa kwa amani na utulivu.


Aidha amesema amewataka madereva baadhi ya ambao ni watumiaji wa pombe,  kuacha kutumia vilevi huku wakiendesha vyombo vya moto, atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ameongeza katika kipindi hiki cha Sikukuu, vikosi mbalimbali vya jeshi hilo, vitakuwa vikifanya doria wakati wote vikiwemo vikosi vya mbwa na farasi.


No comments:

Post a Comment