AAHIDI YA SH. MIL 100 YATOLEWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA SARANGA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 9, 2025

AAHIDI YA SH. MIL 100 YATOLEWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA SARANGA


NA MWANDISHI WETU


SHILINGI Milioni 100 zimeahidiwa kutolewa kwa lengo la kukamilisha  ujenzi wa Kituo cha Afya kilichopo Kata ya Saranga , Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amefunguka hayo leo Aprili 9, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo akiwa katika ziara yake katika Jimbo la Kibamba kukagua miradi ya maendeleo.


Pia ametabaisha kuwa fedha hizo zitawalishwa wiki ijyao ili ziweze kukamilisha jengo la Kituo cha Afya ambacho kinaaminika kitasaidia kuwahudumia wakazi wa eneo hilo.


"Naomba niseme hapa kwa maana unaposema ukweli unakuweka huru, wiki ijayo nitafika hapa kwaajili ya kukabidhi fedha hizo pia niwape majibu kwamba katika kipindi hiki wakija wanasiasa wengine hapa kusema Serikali haijafanya kitu, waambieni kwanza waweke fedha kuchangia miradi ya maendeleo,"amesema.

Pia amesisitiza kwamba katika sekta ya afya, Serikali imefanya makubwa chini ya Rais, Samia Saluhu Hassan kwa kuwekeza vifaa Tiba katika hospitali nyingine nchini zinazosaidia kuhudumia watanzania na wageni.

Chalamila ametolea mfano katika Hospitali ya Ocean Road ambayo inatoa matibabu kwa wagonjwa kansa kwamba kuna mashine inayogundua ugonjwa huo ikiwa katika hatua za mwanzo ambayo imenumuliwa kwa zaidi Shilingi milioni 30.

Aidha ukiachana na mashine hiyo, Serikali kununua kwa ajili ya matibabu ya kansa, pia kwa sasa katika hospitali kubwa hapa nchini kuna mashine za CT Scan,ambapo awali ilikuwa ilitolewa, Muhimbili pekee na hiyo inafanya wagonjwa wa mikoani kupata huduma hiyo wakiwa hukohuko bila kufika Dar es Salaam

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameongeza kuwa Serikali imefanikisha ujenzi wa vituo vya afya karibu kila.kata  nchini hivyo ni jambo la kumpongeza Rais Samia, kwa kujali maisha ya watanzania


Pia ameongeza kuwa mchakato wa ujenzi wa barabara ya Saranga  hupo katika hatua za awali na wananchi wote ambao watapitiwa na mradi huo watalipwa fidia.


"Tayari mchakato wa kwanza wa kufanya tathimini imeshafanyika na imeshafahamika nani na nani  wanatakiwa kuondoka na watalipwa fidia kutokana na kupitiwa na mradi huo," amesema.


Chalamila amebainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa michakato mbalimbali kukamilisha mradi huo kwa mwaka huu itakuwa ngumu kukamilika.

Katika mkutano huo, wakazi mbalimbali wa Kata ya Saranga walitoa kero zao,.ambazo zilijibiwa na Mkuu huyo wa Mkoa.





No comments:

Post a Comment