![]() |
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama ametoa pongezi za dhati kwa Dkt. Godwin Mollel kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, hususan katika Sekta ya Afya. Dkt. Mollel ametajwa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na juhudi zake, weledi wake na moyo wa kujitolea unaoendelea kuleta matokeo chanya katika Wizara hiyo.
Kupitia uteuzi wa Rais, Dkt. Mollel ameonyesha uwezo wa kipekee katika kusimamia na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa. Waziri Mhagama amesema kuwa ana imani kubwa kuwa mwaka 2025 utakuwa wenye mafanikio makubwa zaidi kwa sekta ya afya na kwa Watanzania wote.
“Tunamshukuru sana Dkt. Mollel. Tunamtakia kila la heri na tunaamini ataendelea kuleta mwanga katika huduma za afya,” alisema Waziri Mhagama
No comments:
Post a Comment